13 Juni 2025 - 16:53
Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu: Utawala wa Kizayuni Lazima Usubiri Adhabu Kali – Mkono wa Nguvu wa Jeshi la Iran Hautauacha Salama

Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu: Mkono wa Nguvu wa Jeshi la Kiislamu Hautauacha Utawala wa Kizayuni - Kwa idhini ya Mwenyezi Mungu

Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Taarifa kwa Umma wa Iran toka kwa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu Kufuatia Jinai ya Israel Dhidi ya Iran. Ifuatayo ni andiko kamili la Taarifa hiyo:
 

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu

Enyi Taifa Tukufu la Iran!

Katika alfajiri ya leo, mfumo wa Kizayuni umefanya jinai nyingine dhidi ya nchi yetu pendwa, kwa kuonyesha wazi asili yake ya uovu na uadui kwa kulenga maeneo ya makazi ya kiraia. Kwa kufanya hivyo, mikono yao michafu na yenye damu imejifichua zaidi kuliko ilivyokuwa hapo awali.

Mfumo huu dhalimu lazima utarajie adhabu kali.
Na mkono wenye nguvu wa vikosi vya kijeshi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hautauacha - kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.

Katika mashambulizi haya ya kinyama, baadhi ya makamanda na wanasayansi wetu wamepata shahada. Hata hivyo, warithi na wenzao wataendelea mara moja na kazi zao - InshaAllah.

Kwa jinai hii, mfumo wa Kizayuni umejiandalia mwisho mchungu na wenye maumivu makubwa, ambao bila shaka utaupata.

Sayyid Ali Khamenei

13 Juni 2025.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha